Wito wa kuchukua hatua
fotoapelswahili1.jpg

All Together in Dignity  .............. Wito wa kuchukua hatua

Shirika la Kimataifa atd Dunia ya nne pamoja na Kamati ya Kimataifa ya Oktoba 17, tunakukaribisha kujiunga nasi kutoa ahadi katika kuunga mkono mwito huu wa kuchukua hatua :

Katika kipindi cha changamoto zisizotarajiwa, zinazohitaji utekeleazaji wa pamoja hatukubali kupoteza nguvukazi watu zinazowakilishwa na umaskini.

Umaskini ni aina ya vurugu. Matokeo yake ni uonevu na udhalilishaji na hivyo watu kunyamazishwa. Unaharibu maisha na ni kizingiti kikubwa dhidi ya kuelekea katika dunia endelevu yenye amani.

Lakini siyo kwamba umaskini hauzuiliki. Kama ilivyo kwa utumwa na ubaguzi, umaskini unaweza kutokomezwa. Katika muda wote ambao umaskini umekuwepo, wale wote unaowataabisha wamestamili udhalimu. Dunia inahitaji ufahamu na akili zao ili kuweza kukabiliana na changamoto za leo.

Umewadia wakati wa kujenga dunia ambayo hakuna anayeachwa nyuma.Kwa kujifunza kutoka kwa wale wanaoishi katika umaskini, hatimaye tunaweza kujiweka huru kutoka katika kutengwa na kumilikiwa, hali ambayo imekuwa ikitawala mahusiano ya kibinadamu kwa muda mraefu.

Tangu Oktoba 17 1987, adhimisho la kwanza la Siku ya Kutokomeza Umaskini Duniani lilipofanyika, watu kutoka katika nyanja zote za maisha na mashirika yasiyohesabika yameitikia mwito wenye nguvu uliozinduliwa na Joseph Wresinski, muasisi wa ATD Dunia ya Nne.

Popote pale wanaume na wanawake wanapohukumiwa kuishi katika umaskini, haki za binadamu zinakiukwa. Kujiunga pamoja kuhakikisha kwamba haki hizi zinaheshimiwa ni wajibu wetu muhimu.

Mwito huu ni jibu ambalo lisilo la vurugu kwa vurugu za umaskini. Umewezesha idadi ya watu wasiohesabika wanaoishi katika umaskini kupaaza sauti zao, kutenda pamoja na wengine na kusikika.

Kila mwaka, pote duniani, watu zaidi na zaidi kutoka aina tofauti za maisha wamejiunga pamoja kuukataa umaskini kwa kushinikiza haki za msingi za binadamu ziheshimiwe na kusisitiza mashirika na taasisi kuchukua hatua. Kila mara juhudi zote hizi zimethibitisha kwamba tunaposhirikiana pamoja tunaweza kushinda hali ya kutengwa na umaskini.

Tukishirikiana pamoja, inawezekana kujenga dunia ambayo tutawweza kuishi kwa amani, iliyo huru dhidi ya umaskini na uoga, mahali ambapo binadamu wote wanaweza kufikia malengo yao kikamilifu.

(cliquez sur l'image pour signer l'Appel sur le site: stoppauvrete.org )

Leer también