Commemorative stone
dalle_paris_2012

Siku ya tarehe 17 Oktoba 1987, kwa kuitikia mwito wa Joseph Wresinski, idadi ya watu 100,000 ambao ni watetezi wa haki za binadamu, walikusanyika pamoja katika jijini Paris (Ufaransa) kuonesha jinsi watakavyoukataa umaskini uliokithiri, kwa kuwataka wanadamu wote kujiunga pamoja na kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinaheshimika.

ATD Fourth World

"Popote pale wanaume na wanawake wanapohukumiwa kuishi katika umaskini uliokithiri haki za binadamu zimevurugwa. Kuungana pamoja ili kuhakikisha kwamba hizi haki zinaheshimiwa ni jukumu letu sote.“

JOSEPH WRESINSKI

TJiwe la kumbukumbu linaloelezea ujumbe huu lililozinduliwa katika tukio hili mahali ambapo sasa hivi panaitwa “Human Right and Liberties Plaza” mahali ambapo tamko kuu la Ulimwengu la Haki za Binadamu liliposainiwa mnamo mwaka 1948.

Hao watu 100,000 waliokuwa wamehudhuria walikuwa wananchi kutoka nyanja na hali mbalimbali za maisha. Baadhi yao waliwakilisha ngazi za juu za kimataifa, kitaifa, na tawala mbalimbali za serikali za mitaa. Wengine walikuwa watu binafsi na familia ambazo wenyewe wanaishi katika ufukara sugu wakipambana nao katika maisha ya kila siku.

Commemorative Stone
Commemorative Stone

Tangu hapo, kila mwaka, siku ya tarehe 17 Oktoba, wale wote wanokataa umaskini uliokithiri na kutengwa pamoja na maskini wenyewe,    hukusanyika    kote    ulimwenguni    na    kuonesha mshikamano wao na ushirikiano kwa dhati kuhakikisha kwamba heshima na uhuru wa kila mmoja vinaheshimiwa. Huu ulikuwa mwanzo wa Siku ya Kimataifa ya Kuushinda Umaskini Uliokithiri.

Mnamo tarehe 17 Oktoba, 1992, Bw. Javier Perez de Cuellar, aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa, kwa niaba ya kundi la watu maarufu wa kimataifa alikutana katika kamati ya Siku ya Kimataifa ya Kuushinda Umaskini Uliokithiri na alitaka siku hii ya tarehe 17 Oktoba itambuliwe. Mnamo tarehe 22 Desemba 1992, Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa ulitamka na kuifanya siku hii kuwa “Siku ya Kimataifa ya Kuushinda Umaskini Uliokithiri.” Tangu hapo, juhudi za kuifanya siku hii itambulike zimekuwa zikiongezeka.

Discover the replicas of the Commemorative Stone around the world.